Djuma aahidi kuisuka upya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
25 Dec 2017
Djuma aahidi kuisuka upya Simba
Kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma, amewaambia wachezaji wa Simba kuwa anatarajia kufanya mambo matatu kwao na lazima wajipange.

Djuma alisema mambo aliyopanga kwa wachezaji hao ni kuwapa mifumo mitatu mipya ya uchezaji itakayotoa nafasi kwa wachezaji wote kucheza, lakini pia atakazia zaidia suala la nidhamu ili kuifanya Simba izidi kupaa.

Lakini kubwa alilosisitiza ni kwamba kuanza sasa wachezaji hao wajiandae kisaikolojia kwani amepanga kuvunja ustaa ndani ya timu.

Baadhi ya nyota wa Simba walithibitisha juu ya mambo hayo matatu ambayo kocha Djuma ameanza nayo fasta baada ya kupewa mikoba ya ikocha mkuu.<

Wachezaji hao walisema ni kweli Mrundi huyo tayari amewapa maelekezo hayo ambayo ataanza kuyafanyia kazi mara moja.

“Ametuambia kuwa kwa sasa ndani ya timu hakuna staa na kila mchezaji atacheza, ataanza na mifumo mitatu itakayotoa fursa kwa wote, huku akisisitiza nidhamu,” alisema mmoja wa wachezaji waandamizi wa Simba.

Kocha Djuma alisema anaanza kurudisha heshima ya klabu ya Simba na morali kwa mashabiki na wanachama kwa kuifunga Ndanda FC kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mjini Mtwara.

“Nafahamu mashabiki na wanachama wamepoteza imani na timu yao, lakini nitahakikisha imani yao inarejea na hiyo ni kushinda mechi zijazo, tunachopaswa kukifanya sasa ni kusahau yaliyopita na kuangalia yaliyopo mbele yetu. Bado timu ni nzuri na kikosi ni kipana,”.

Djuma alisema katika mazoezi ya jana Jumapili asubuhi alitumia muda wake kuzungumza na wachezaji ili kila mmoja kujua jukumu lake ndani ya timu.

“Nataka kila mmoja aelewe jukumu lake uwanjani, kwani tunachohitaji sasa ni ushindi pekee na si kitu kingine, hivyo Wana Simba wategemee baadhi ya mabadiliko yenye mafanikio katika timu,” alisema Djuma.

Djuma alisema mipango yake ni kurejesha Simba katika kiwango bora kwani anafahamu kiu ya Wanasimba wote ni mafanikio na kutwaa ubingwa wa VPL

“Kuhusu suala la nidhamu Simba ni jambo la ndani sana si kulitoa nje, ila binafsi napenda mchezaji afahamu majukumu yake mambo mengine. Nidhamu ni kitu cha msingi sana katika timu,” alisema Djuma.

“Omog alikuwa ni bosi wangu na nilimkuta ana mfumo wake japo wakati mwingine tulijadiliana, ila mimi nina mfumo wangu huo ambao mara nyingi napenda kuutumia, “alisema

Djuma ambaye amewataka mabosi wa Simba kumtafutia uwanja mwingine wa mazoezi kwani anasema ule wa Chuo cha Polisi, Kurasini sio mzuri kwa timu yake kujinoa hapo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →