Manula hana kinyongo kutemwa Stars, ampa tano Kaseja

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2019
Manula hana kinyongo kutemwa Stars, ampa tano Kaseja

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amemtakia kila la kheri mkongwe Juma Kaseja katika mchezo wa kesho dhidi ya Sudan

Kaseja aliyerejeshwa timu ya Taifa na Kaimu Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije, ameendelea kuaminiwa akidaka mechi zote za hivi karibuni

Kaseja aliitwa kuchukua nafasi ya Manula ambaye mwanzoni mwa msimu alikabiliwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa

Katika kikosi cha Stars kitakakochoivaa Sudan, walinda lango wote wa Simba Manula na Beno Kakolanya hawakujumuishwa kwenye kikosi hicho

Uamuzi huo ulizua mjadala mkali miongoni mwa wadau wa soka nchini wengi wakiamini Manula alistahili kurejeshwa Stars hasa baada ya kuwa amepona majeraha

Wakati mjadala huo ukiendelea, Manula amesema Kaseja ni kipa mzoefu, anamuheshimu na kama Taifa wote tunapaswa kuwaunga mkono wachezaji wa Stars kwani wanawakilisha nchi

"Unapozungumzia timu ya taifa maana yake umegusa Watanzania wanaohitaji matokeo mazuri, nawaombea baraka kwa wote walioitwa Stars wakafanye kazi kubwa"

"Sina wasiwasi na Kaseja, ameaanza muda mrefu kudaka kabla yangu na mafanikio yake yameonekana namtakia baraka tele akafanye vizuri kwa niaba ya Watanzania, " amesema

Manula alisema kwa sasa akili yake imezama zaidi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Kipa huyo alisema anahitaji kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya na vizuri na hatimaye kutetea taji lao.

Alisema watataendelea kupambana ili mwakani waweze kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mwaka huu, kutolewa hatua ya awali na timu ya UD Songo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’