Tutatetea ubingwa kwa msimu wa tatu - Manula

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Sep 2019
Tutatetea ubingwa kwa msimu wa tatu - Manula

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amesema wamedhamiria kuchukua ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Manula aliyerejea kikosi mwanzoni mwa msimu baada ya kupona majeraha, amesema anaamini wana kikosi imara kitakachoweza kutwaa ubingwa

Amesema kila mchezaji aliyesajiliwa na Simba, ana uwezo wa kupambana na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo watacheza.

"Kiwango cha timu yetu hakikuwa duni, kwa namna mechi zetu mbili za mwanzo tulizocheza, tumecheza vizuri, nadhani tutaendelea kupambana katika mechi zote ili tutimize malengo yetu," alisema Manula.

Aliongeza kwamba wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea katika kikosi hicho, na wameendelea kuifanya timu hiyo kuonekana kuwa na mwanzo mzuri wa msimu.

Simba imeshinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya JKT Tanzania (3-1) na Mtibwa Sugar (2-1)

Inaendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Septemba 26 uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’