Matola amtabiria makubwa Miraji Athumani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Sep 2019
Matola amtabiria makubwa Miraji Athumani

Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Selemani Matola amesema winga Miraji Athumani atapata mafanikio baada ya kurejea Simba kwa mara ya pili

Matola ndiye aliyekuwa mkufunzi wa Lipuli Fc msimu uliopita, Miraji akiwa mmoja wa wachezaji wa kikosi chake

Matola pia aliwahi kuwa kocha wa Simba B akijivunia kuwaandaa nyota kadhaa wa Simba akiwemo Miraji, Ibrahim Ajib, Jonas Mkude, Said Khamis Ndemla na Mohammed Hussein

Matola amesema anamfahamu Miraji kama mchezaji anayependa kujituma na kupata mafanikio

"Miraji anajitambua na ni mtu ambaye anapenda mafanikio, kwa hiyo kutokana na kuwa na roho hiyo naamini kabisa kuwa, kasi aliyoanza nayo ndiyo hiyo atakayoendelea nayo kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote," amesema Matola ambaye anamnoa winga huyo timu ya Taifa

Akizungumzia ushindani wa namba kwenye kikosi cha Simba, Matola amesema anaamini Miraji atapewa nafasi ya kocha Patrick Aussems kwani ni mchezaji mwenye uwezo

Miraji tayari amefunga mabao mawili msimu huu katika michezo ya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’