Mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar,Azam FC ambaye pia amewahi kuitumikia timu ya Taifa, Ibarahim Rajab 'Jeba' amefariki dunia katika Hospital ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Jeba alikuwa ameanza mazoezi na timu yake ya Chuoni kwa ajili ya kurejea kucheza ligi kuu ya Zanzibar baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda.
Chuoni Fc imethibitisha kifo cha kiungo huyo aliyewahi kutamba ligi kuu ya Tanzania Bara

Jeba alitamba katika kikosi cha Mtibwa Sugar kilichowatoa nyota kama Andrew Vicent (Yanga), Shiza KIchuya (ENPPI-Misri) na Mzamiru Yassin (Simba)
Pumzika kwa Aman fundi wa mpira..
ADVERTISE HERE