Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hawawezi kurudia makosa yaliyopelekea msimu uliopita wapoteze michezo yote miwili dhidi ya Kagera Sugar
Septemba 26 Simba itasafiri mkoani Kagera kuwakabili Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba
Kagera Sugar ni moja ya timu ambazo zimekuwa zikiipa changamoto Simba katika misimu ya hivi karibuni
Aussems ambaye anakiandaa kikosi chake uwanja wa Gymkhana, amesema msimu huu hawatakubali kufungwa na Kagera Sugar
"Tunajiandaa vyema kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo. Najua tunakwenda kucheza na timu ambayo msimu uliopita ilitufunga mechi zote mbili, lakini huu ni msimu mwingine, hatutarudia makosa ya msimu uliopita," alisema
Simba inaendelea kujifua bila ya nyota wake nane ambao wameitwa timu ya Taifa ya Tanzania inayohusisha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mchezo dhidi ya Sudan Jumapili