Aussems apania kukoleza 'moto' wa washambuliaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Sep 2019
Aussems apania kukoleza 'moto' wa washambuliaji Simba

Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Mbelgiji Patrick Aussems, amesema ataendelea kuwanoa washambuliaji wake ili waweze kufunga mabao mengi zaidi katika mechi zinazofuata

Aussems ambaye tayari timu yake imefunga mabao matano msimu huu, amesema anahitaji kuona safu yake ya ushambuliaji inatumia vema nafasi za kufunga wanazozitengeneza na hatimaye kupata ushindi mnono katika kila mechi watakayocheza.

Aussems alisema kila mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ni ngumu, na ili kujiweka katika nafasi salama zaidi ni kupata mabao mengi ambayo yatawahakikishia kuondoka na pointi tatu.

"Nawapongeza kwa kucheza vizuri na kupata ushindi katika mechi mbili tulizocheza za Ligi Kuu, lakini bado hawatumii vizuri nafasi ambazo wametengeneza, katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, wamepoteza nafasi kama tatu nyingine za kufunga, tunahitaji kulimaliza tatizo hili," Aussems amenukuliwa na Nipashe

Aliongeza kuwa anahitaji kuona hawarudii makosa katika mechi ijayo dhidi ya Lipuli Fc na kupata ushindi ili kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.

Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Hussein "Zimbwe Jr" amesema kikosi chao kina kiu ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu mwingine wa tatu mfululizo.

"Tunajua hakuna mechi rahisi, timu zote zimejiandaa kuonyesha ushindani, kila mchezo kwetu tunauona kama fainali, naamini tutaendelea kupambana ili tutimize malengo yetu, tunaomba ushirikiano uliokuwapo, uendelee," Zimbwe Jr alisema.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania na Ijumaa ilipata ushindi wa mabao 2-1 walipoikaribisha Mtibwa Sugar kutoka Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’