Nahodha wa Simba John Bocco anaendelea kuimarika baada ya kuanza mazoezi mepesi akitoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa mwezi mzima
Habari njema ni kuwa Bocco huenda akarejea dimbani kwenye mchezo ujao wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Lipuli Fc
Simba na Lipuli zitachuana dimba la Uhuru siku ya Jumapili, Septemba 22 2019
Bocco hajaonekana kwenye kikosi cha Simba kwa muda sasa akiuguza majeraha aliyopata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba August 17
Simba imeweza kushinda mechi mbili za kwanza licha ya kumkosa
Meddie Kagere na Miraji Athumani wamefunga mabao matano (Kagere (3), Miraji (2))
ADVERTISE HERE