Kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wa Simba baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1
Ulikuwa ni mchezo ambao kama safu ya ushambuliaji ingekuwa makini, ushindi mnono zaidi ungepatikana, kocha Patrick Aussems aliligusia hilo
Hata hivyo kuna baadhi ya nafasi zilipotezwa kutokana na wachezaji kukosa kushirikiana
Kiungo fundi Clatous Chama jana alipoteza nafasi kadhaa lakini pengine kama angewapasia wenzie mpira wangeweza kufunga
Muhimu Wanamsimbazi walihitaji ushindi na ulipatikana lakini suala la wachezaji kushirikiana linafaa lizingatiwe
Chama amekuwa akifanya vizuri sana kwenye kikosi cha Simba tangu aliposajiliwa msimu uliopita, lakini wakati mwingine maamuzi yake yamekuwa yakiikosesha timu mabao
Tangu kuanza kwa msimu huu, Chama anaonekana kutaka kufunga kila anapopata nafasi ya kuelekea langoni ingawa wakati mwingine angeweza kuwapasia wenzie walio kwenye nafasi nzuri zaidi
Hili ni jambo ambalo wachezaji wa Simba wanapaswa kukumbushwa