Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho Ijumaa kinashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuikabili Mtibwa Sugar ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ligi kuu ya Vodacom
Mabingwa hao watetezi wana kazi moja tu, kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika kampeni ya kulirejesha kombe Msimbazi kwa msimu wa tatu mfululizo
Msimu uliopita Simba iliifumua Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Kocha Patrick Aussems amesema licha baadhi ya nyota wake kukosekana, wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, inaelezwa wachezaji wa Simba wamejiwekea malengo ya kutopoteza mchezo kwenye ligi msimu huu
Simba ilianza msimu kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania wakati wapinzani wao Mtibwa Sugar walianza msimu kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Lipuli Fc