Adrian Chota Chama (ACC) ni kaka wa kiungo mahiri wa Simba Clatous Chota Chama ( CCC)
Adrian ni beki wa kutumainiwa wa kikosi cha ZESCO ambacho wakati wowote kitawasili nchini kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi
Familia na Mzee Chota imebarikiwa kuwa na vijana hao ambao wana vipaji vya hali ya juu katika kusakata kabumbu
Wote wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia
Uwepo wa Chama kwenye kikosi cha ZESCO huenda ukaongeza hamasa kwa mashabiki wa Simba ambao siku ya Jumamosi wameapa kuwa bega kwa bega na ZESCO United
ADVERTISE HERE