CEO mpya aongeza mzuka Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Sep 2019
CEO mpya aongeza mzuka Simba

Siku chache tangu uongozi wa klabu ya Simba kumtambulisha bosi mpya, kitendo hicho kimelipandisha mzuka benchi la ufundi ambalo limeapa kukisuka zaidi kikosi ili kiwe na makali ya kufanya mauaji katika mechi zao zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wikiendi iliyopita, Simba walimtambulisha rasmi Senzo Mazingisa, raia wa Afrika Kusini, kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) baada ya Crescentius Magori, kumaliza muda wake.

Moja ya vitu ambavyo Mazingisa, alivyovingumza katika utambulisho wake, ni kuifanya Simba kuwa klabu bora Afrika kulingana na makubaliano ya mkataba wao.

Kauli hiyo ya Mazingisa inaonekana kuanza kufanyiwa kazi na benchi la ufundi ambalo linataka kusuka kikosi cha maangamizi kuelekea mechi zao za  Ligi Kuu Bara na michuano yoyote itakayopita mbele yao.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam, inadhihirisha hilo kwa sababu ya aina ya tizi walilokuwa wanapewa wachezaji wa timu hiyo.

Licha ya uwepo wa wachezaji wachache mazoezini kutokana na wengine kuwa na majukumu ya timu zao za Taifa, Kocha Mkuu Patrick Aussems, alikuwa makini kuhakikisha kila mmoja anafanya kile anachotaka.

Wekundu wa Msimbazi hao, walikuwa wakifanya mazoezi ya aina tofauti, zaidi ikiwa yale ya kuongeza pumzi na kasi ya kukimbia wanapokuwa uwanjani.

Wacheza walikuwa wanakimbia kwa zamu huku wamefunga vifaa vya kuwafanya kuwa na kazi pamoja na pumzi, kocha akiwa amewasimamia, wakipokezana.

Kocha Patrick Aussems, aliweka bayana kuwa lengo kwa sasa baada ya kupitia kipindi kigumu cha kuondolewa katika michuano ya kimataifa, anataka kuwadhihirishia wapenzi wa soka kuwa kikosi chao ni bora.

Aussems alisema kutokana na maandalizi wanayofanya, ubora wao utaanza kuonekana katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar inayotarajia kuchezwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Alisema mechi yao imerudishwa nyuma, tofauti na simu waliyotakiwa kucheza, lakini hilo halimpi presha kwani msimu huu wamejipanga na kitendo cha ratiba hiyo kubadilika hakijaathiri chochote.

“Tumeendelea na mazoezi kwa wachezaji ambao hawapo katika timu za Taifa, nafurahi kikosi kipo vizuri tumejipanga kukabiliana na Mtibwa Sugar, tena imerudishwa tunacheza Ijumaa, hiyo haina tatizo.

“Haya mazoezi ya mbio tuliyoyafanya leo(jana), ni kuwaweka  wachezaji vizuri, mengine yamepita na sasa tunaangalia mbele kuonyesha kila mtu kwamba sisi ni timu bora na hilo litaanzia siku ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema Aussems.

BINGWA

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’