Mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere bado hajarejea kutoka Rwanda anakokabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa
Wiki iliyopita Kagere aliisaidia Rwanda kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi kombe la dunia kwa upande wa Afrika
Rwanda itarudiana na Shelisheli kesho
Wakati Kagere akikabiliwa na majukumu hayo ya timu ya Taifa, nahodha John Bocco bado ni majeruhi akiendelea na matibabu ya majeraha aliyopata August 17 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC
Katika mazoezi ya leo, kocha Patrick Aussems alionekana kumuandaa mshambuliaji Deo Kanda kuongoza safu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Uhuru Ijumaa ya wiki hii
Mchezo dhidi ya Mtibwa ambao awali ulipangwa kupigwa Septemba 17, umerudishwa nyuma hadi Septemba 13