Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 09 amemkabidhi mlinda Mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja kitita cha Shilingi Milioni 10 ikiwa ni sehemu ya Motisha na zawadi ya Kazi nzuri aliyoifanya jana wakati wa Mchezo dhidi ya Burundi.
RC Makonda amemkabidhi Kaseja fedha hizo mbele ya Kocha wa Taifa Stars, Katibu Mkuu wa TFF na baadhi ya wachezaji waliomsindikiza ambapo amekipongeza kikosi kizima cha Timu ya Taifa kwa kututoa kimasomaso kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022
Makonda aliahidi kutoa zawadi hiyo kwa Kaseja jana baada ya mchezo
ADVERTISE HERE