Nimerudi kuwapa furaha mashabiki Simba - Ajib

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Sep 2019
Nimerudi kuwapa furaha mashabiki Simba - Ajib

Kiungo fundi wa Simba Ibrahim Ajib amesema anaanza rasmi kazi kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara baada ya kupona majeraha

Ajib alianza msimu kwa kusuasua akipata majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki tatu akikosa mechi za ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo

Hata hivyo 'Mzee wa Makorokoro' amepona kabisa na mechi ya kwanza ya Simba ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania alipewa dakika chache

Ajib aliyekuwa kinara wa kupika mabao akiwa na Yanga msimu uliopita, amesema kazi hiyo ataiendeleza Msimbazi

"Nilikuwa majeruhi lakini sasa nimepona, nashukuru naendelea kuimarika kadiri ninavyofanya mazoezi," amesema

"Wanasimba watulie, nimekuja kufanya kazi. Naamini mafanikio niliyopata msimu uliopita nitayaleta hapa.."

Hata hivyo Ajib anapaswa kujituma kwelikweli ili kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kwani ushindani wa namba ni mkali

Ajib anakabiliwa na upinzani kutoka kwa nyota kama Hassan Dilunga, Francis Kahata, Deo Kanda na Clatous Chama

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’