Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo kitashuka dimba la Taifa kurudiana na Burundi katika mchezo wa hatua za awali kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia
Timu hizo zilicheza siku tatu zilizopita nchini Burundi na kutoka sare ya bao 1-1
Ushindi au matokeo ya suluhu ya bila kufungana kwa Tanzania, yatatosha kuihakikishia kucheza hatua ya makundi
Mashabiki wameaswa wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuwaunga mkono Stars katika mchezo huo
Viingilio vya mchezo, Mzunguuko ni Tsh 2000/- na VIP ni Tsh 5000/-, lengo ni kuhakikisha mashabiki wanajaza uwanja wa Taifa
Nahodha wa Stars Mbwana Samatta amesema wamejiandaa na wana matumaini ya kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa kumi jioni
ADVERTISE HERE