Tushirikiane kuifanya Simba iwe klabu kubwa Afrika - CEO Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Sep 2019
Tushirikiane kuifanya Simba iwe klabu kubwa Afrika - CEO Simba

Mtendaji Mpya wa klabu ya Simba Senzo Mazingiza amewataka Wanasimba kuendelea kushirikiana ili kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika

Mazingiza ametambulishwa leo na uongozi wa Simba akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye amemaliza muda wake

Akizungumza baada ya utambulisho huo uliofanyika Hotel ya Serena, Mazingiza amesema Simba ni klabu kubwa Tanzania yenye historia ya kipekee ukanda wa Afrika Mashariki

Amewataka Wanasimba kuendelea kushirikiana ili kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa barani Afrika

"Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa naifatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika," amesema

Aidha, Mazingiza ameeleza kufurahishwa na mwamko wa mashabiki wa Simba na kuwataka waendelee kuiunga mkono timu yao wakati wote

"Nilikuwa hapa simba day nilishangazwa na mashabiki wengi waliojitokeza naomba tuendelee hivi hivi siku zote tuisapoti timu"

Naye CEO aliyemaliza mda wake Crescentius Magori, amewashukuru Wanasimba wote kwa sapoti waliyompa kipindi chote alichokuwa katika nafasi hiyo

"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa. Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu."

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’