Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Wilfredy Kidao amewataka watanzania kuendeleza sifa ya ushangiliaji kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kushiriki hatua ya makundi ya Kombe la Dunia dhidi ya Burundi utakaofanyika Jumapili ya wiki hii Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika mkutano na kamati ndogo ya hamasa ya Taifa Stars, Kidao amesema, Tanzania imekuwa na sifa ya kipekee kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) linapokuja suala la ushabiki hivyo ni wajibu wetu kuiendeleza sifa hiyo
"Kama tunavyoonwa huko na wenzetu, lakini inawezekana sisi hatutambui fursa tuliyonayo kwahiyo tusiache thamani tunayopewa, rai yangu Watanzania mjaze Uwanja, "amesema
"Tunasema kila mtu na wajibu wake, sisi kazi yetu ni kushangilia na vijana yaani wachezaji kazi yao ni kucheza kwa bidii ili kupata ushindi kwa hiyo sisi tutakapo hamasishana kwa nguvu zetu wachezaji watakuwa na deni na haijawahi kutokea Uwanja wa Taifa ukajaa halafu mgeni atoke salama