Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Burundi kuwa ni Tsh 2,000/- kwa mzunguko na Tsh 5,000/- kwa eneo la watu mashuhuri (VIP).
Taifa Stars inatarajia kuwa mwenyeji wa Burundi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Bunjumbura, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1
Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema wameshusha bei za viingilio ili kuwapa fursa mashabiki wengi kwenda kuipa nguvu Taifa Stars
Kuelekea mchezo huo, mashabiki wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa keshokutwa ili kuiunga mkono Stars inayosaka nafasi ya kucheza makundi kwenye kinyan'ganyiro cha kuwania nafasi tano za michuano ya kombe la dunia kwa upande wa Afrika
Jumapili Stars inahitaji matokeo yoyote ya ushindi au hata suluhu ya bila kufungana