Kiungo Said Khamis Ndemla amesema anatumia muda wake wa ziada kufanya mazoezi ili kuhakikisha anakuwa fit ili amshawishi kocha Patrick Aussema ampe nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Ndemla hakuwa na mwanzo mzuri msimu huu akikabiliwa na changamoto ya kupata nafasi kutokana na ushindani mkali wa namba kwenye nafasi ya kiungo
Ndemla amesema anafahamu changamoto itakuwa kubwa zaidi hasa baada ya Simba kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
"Nimekuwa nikifanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha namshawishi Mwalimu anipe nafasi," amesema
"Ushindani ni mkubwa na utaongezeka baada ya kuwa tumetolewa kwenye ligi ya mabingwa"
"Haitakuwa rahisi kupata namba ndani ya kikosi cha kwanza kutokana na ubora wa kikosi hivyo ni lazima nipambane"
Ndemla aliongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba mwezi Julai