Mshambuliaji Adam Salamba alikuwa na ndoto kubwa ya kwenda kucheza nje ya nchi
Salamba aliyetua Simba akitokea klabu ya LIpuli Fc, msimu wake mmoja Msimbazi haukuwa na mafanikio kutokana na ushindani mkubwa wa namba
Alipata nafasi kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini kunako klabu ya TS Sporting
Hata hivyo dili la kutua timu hiyo lilikwama hivyo kulazimika kurejea nchini na Simba kumtoa kwa mkopo klabu ya Namungo Fc
Hakukata tamaa, na hatimaye juhudi zake zimezaa matunda baada ya kupata timu Kuwait
Amesajiliwa na Al Jahra Sc, akisaini mkataba wa miaka mitano
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, atakuwa miongoni mwa nyota wa kigeni wanaolipwa vizuri kwenye klabu hiyo
Atakuwa na uhakika wa kupokea sio chini ya Mil 10 kwa mwezi
Salamba anatoa somo kwa wachezaji wengine kuwa, ukijiwekea malengo unaweza kufanikiwa kama utawekeza juhudi na maarifa kutimiza malengo hayo