Mshambuliaji wa Simba Adam Salamba yuko mbioni kujiunga na Al Jahra Fc inayoshiriki ligi kuu ya nchini Kuwait
Salamba ambaye alitolewa kwa mkopo kuitumikia klabu ya Namungo Fc kwa mwaka mmoja, ameondoka nchini baada ya kupata ofa hiyo
Inaelezwa Al Jahra imefikia makubaliano na Simba ambapo italipa fedha zinazokaribia Tsh Milioni 100 kumnunua
Kama mambo yakienda sawa, Salamba atasaini mkataba wa miaka mitano ambao utamfanya alipwe wastani Tsh Milioni tisa kwa mwezi
ADVERTISE HERE