Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amemsifia mshambuliaji wa timu hiyo kinara wa mabao Meddie Kagere kuwa ni mshambuliaji anayefahamu vyema majukumu yake
Kagere ameanza msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom kwa kupachika mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania
Aussems amesema wakati wote Kagere anafahamu nini afanye ili afunge
"Ni mshambuliaji hatari, muda wote ananusa magoli," amesema
Kagere aliyetua Simba msimu uliopita akitokea klabu ya Gor Mahia, aliweza kufanya mambo makubwa kwenye msimu wake wa kwanza tu, akiibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kufunga mabao 23
Lakini pia alishinda tuzo mchezaji bora wa msimu wa klabu ya Simba pamoja na kuwa miongoni mwa vinara wa upachikaji mabao ligi ya mabingwa
Kagere anatabiriwa kuwa msimu huu atafanya mambo makubwa zaidi