Aussems awataka wachezaji waongeze 'dozi' ya vipigo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Sep 2019
Aussems awataka wachezaji waongeze 'dozi' ya vipigo

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa anataka kuona timu yake inapata ushindi wa mabao kuanzia matatu hadi matano kwenye michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 walipokutana na JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Alhamisi iliyopita.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere aliyefunga mawili kabla ya Athumani Miraji kuingia katika kipindi cha pili na kufunga moja.

Aussems alisema licha ya vijana wake kucheza vizuri, lakini hakuridhishwa na idadi ya mabao waliyofunga kutokana na nafasi nyingi walizozipata za kufunga ambazo kama wangekuwa makini wangefunga mabao matano.

Aussems alisema kuwa tayari amekaa na washambuliaji wake Meddie Kagere, Deo Kanda na John Bocco kwa ajili ya kuzungumza nao na kikubwa aliwasisitiza kutumia kila nafasi watakazozipata katika mechi.

Aliongeza kuwa anataka kuona timu inapata ushindi wa mapema ndani ya dakika 15 za mwanzo mara baada ya mchezo kuanza kwa lengo la kuwavuruga wapinzani wao.

"Siku zote unapopata bao la mapema mpinzani wako anachanganyikiwa kwa kucheza kwa presha kubwa, hivyo nimewataka washambuliaji wangu kuongeza umakini wakiwa ndani na nje ya 18 kwa kutumia vema nafasi za kufunga"

"Kama unakumbuka mchezo wetu uliopita wa ligi tulipocheza na JKT, wachezaji wangu walitengeneza nafasi nyingi za kufunga kama wangekuwa makini, basi mchezo huo ungemalizika mapema, basi tungeibuka na ushindi wa mabao matano"

"Na hicho ndiyo kitu kinachokitaka kwani ushindi wa mabao mengi, mwishoni mwa ligi yatakuwa na faida kubwa kama ikitokea tukiwa na pointi sawa, ni matarajio yangu kuwaona wachezaji wakibadilika kwa haraka"

Championi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
5h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
23h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’