Miraji asaka nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Aug 2019
Miraji asaka nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza Simba

Winga mpya wa Simba, Miraji Athuman amesema anachokipigania kwa sasa ni kuhakikisha kocha mkuu Patrick Aussems anamshawishi ili kupangwa kikosi cha kwanza.

Aussems amekuwa akimpa nafasi mchezaji huyo na mechi yao ya ufunguzi alifunga bao moja, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Mchezaji huyo amesema anatamani kufanya kazi na sio kuwa mchezaji wa kusugua benchi, akidai anaamini nidhamu na juhudi ndivyo vitakavyofanya afikie anachokiwaza.

"Huwa najipa moyo kwamba ninaweza licha ya Simba kuwa na wachezaji wazoefu ambao uwezo wao upo wazi, hilo haliwezi kuninyima raha kwamba nitakuwa sipati namba," Miraji aliliambia Mwanaspoti

"Mchezaji ambaye ananifanya nijiamini nitaweza kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kwanza ni Shiza Kichuya alitoka Mtibwa Sugar na akafanya maajabu, hata mimi nitafanya maajabu,"anasema.

Juzi Miraji alifunga moja ya mabao ya Simba kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
8h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’