Kuna wachezaji hawana nyota ya kupendwa na mashabiki wala kuzungumzwa sana na vyombo vya habari, kiungo Mzamiru Yassin anaweza kuwa mmoja wa wachezaji hao
Mzamiru amekuwa katika kiwango bora kwa muda mrefu, ni mmoja wa wachezaji wenye mchango mkubwa sana kwenye kikosi cha Simba
Juzi ni 'assist' zake mbili zilizomuwezesha Meddie Kagere kucheka na nyavu mara mbili
Katika mchezo huo dhidi ya JKT Tanzania pengine Mzamiru alistahili kuibuka kuwa nyota wa mchezo
Mzamiru ni hazina kubwa kwa Simba, kocha Patrick Aussems anafahamu jinsi ya kutumia kiungo huyo aliyetua Simba misimu mitatu iliyopita akitokea Mtibwa Sugar
ADVERTISE HERE