Ujumbe wa Mo Dewji kwa Wanasimba
Wanasimba, mnisamehe kwa ukimya. Maumivu ya matokeo yametupata sote. Naomba tukumbushane: Sisi ni SIMBA! Simba lazima anyanyuke! Hawezi kukata tamaa
Niwaombe tusivunjike moyo wala kukata tamaa. Hatutaogopa maneno ya watu na hatutaacha kupambana na kujipanga kwa ajili ya malengo yetu. Msimu huu tutautumia kikamilifu kuhakikisha tunaboresha mipango yetu ili msimu ujao turudishe furaha kwa Wanasimba wote.
Tumwombe Mwenyezi Mungu atutangulie katika safari yetu endelevu.
Tukumbushane tena: Roma haikujengwa kwa siku moja. Tuwe wavumilivu, tutafika tu Insha’Allah
ADVERTISE HERE