Kagere na hesabu za kiatu cha dhahabu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Aug 2019
Kagere na hesabu za kiatu cha dhahabu

Baada ya Simba kuondolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, straika wao Meddie Kagere amesema akili zao sasa wamezihamishia kwenye ligi kuu kuhakikisha wanatetea ubingwa wao

Simba imeanza ligi vizuri kwa kuifunga JKT Tanzania mabao 3-1 huku Kagere akifunga mabao mawili

Kagere aliyeibuka mfungaji bora msimu uliopita kwa kufunga mabao 23 amesema wachezaji wote wanatakiwa kuweka akili na mawazo yao kwenye ligi ili kuhakikisha wanabaki na ubingwa wao.

"Ukiangalia kwenye ligi kila timu ipo imara hivyo lazima tuwe na malengo na kupambana ili kuhakikisha malengo yetu yanatimia

"Tumeanza vizuri ligi kwa ushindi hivyo tutajitahidi kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo mingine itakayofuata ili tutetee ubingwa"alisema Kagere

Kagere alisema ni mapema mno kuanza kufikiri kutetea kiatu cha dhahabu alichokipata msimu uliopita kwani ligi ni ndefu na ina mambo mengi na hakuna kitu kizuri kama kuwaza kuisaidia kwanza timu yake itetee ubingwa ndipo mambo mengine yafuate

Kagere alifunga mabao 23 msimu uliopita akiwazidi Salim Aiyee ambaye msimu uliopita aliichezea Mwadui Fc akifunga mabao 18 wakati mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo akitikisa nyavu mara 17

Waliofuatia walikuwa ni John Bocco wa Simba aliyefunga mabao 16 na Emmanuel Okwi aliyefunga 15

Makambo hivi sasa ametimkia timu ya Horoya AC ya Guinea wakati Okwi amejiunga na klabu ya Ittihad ya Misri huku Aiyee amejiunga na KMC

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’