Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, watadhihirisha kuwa Simba ndio klabu bora hapa Tanzania
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, Aussems amesema wamesahau matokeo hayo na sasa nguvu zao wamezihamishia kwenye ligi
Aussems amesema ushindi wa leo ni mwanzo wa kudhihirisha umwamba wao katika soka la Tanzania
"Mengine yamepita na sasa tunaangalia mbele kumuonyesha kila mtu kwamba sisi ni timu bora Tanzania na hilo tumeanza leo," amesema
Ushindi wa leo umeifanya Simba iongoze ligi baada ya raundi ya kwanza tu ikiwa sawa na Lipuli Fc ambayo pia iliichapa Mtibwa Sugar mabao 3-1 kwenye mchezo wake wa kwanza
ADVERTISE HERE