Kesho Alhamisi Simba inaanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo ikishuka uwanja wa Uhuru kucheza na JKT Tanzania
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wana kazi moja tu, kuhakikisha wanaanza vizuri msimu
Wakati Yanga leo imeanza kwa kubomolewa bao 1-0 na Ruvu Shooting, ushindi kwa Simba kesho utawaweka mbele mabingwa hao wa nchi kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya watani zao mapema tu
Uongozi wa Simba umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kesho kuiunga mkono timu yao
Baada ya kipindi kigumu cha kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Wanasimba wanapaswa kujitokeza kwa wingi kesho ili kuwaonyesha wachezaji kuwa wako nao
ADVERTISE HERE