Stars yaanza maandalizi ya kuikabili Burundi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Aug 2019
Stars yaanza maandalizi ya kuikabili Burundi

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuingia kambini leo kujiwinda na mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu hatua ya makundi kusaka tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia mwaka 2022

Stars itasafiri kwenda nchini Burundi ambapo Septemba 04 itacheza mechi ya kwanza na kisha timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam Septemba 08

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea vizuri wakishirikiana na serikali kuhakikisha Taifa Stars inaifunga Burundi.

Aidha, alisema kwa upande wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi tayari wamewatumia tiketi zao ili kuja kujiunga na wenzao lengo likiwa ni kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kusonga mbele.

Klabu ya Simba imetoa nyota saba kwenye kikosi cha timu hiyo ambao watajiunga na wenzao baada ya mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania

Walioitwa Stars kutoka Simba ni Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Hassn Dilunga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’