Msemaji wa Simba Haji Manara amesema matokeo ya jana wamewaweka mashabiki katika hali ngumu lakini yabidi kukubali kwani ndio mpira
Manara ambaye jana alisema yuko tayari kuwajibika, amesisitiza utani, dharau, matusi vyote vitapita baada ya muda
"Hakuna kitu kigumu katika maisha ya Soka kwa Wanasimba hususani kwa kizazi hiki cha mitandao ya kijamii kama matokeo ya jana"
"Lakini ndio soka hivyo maisha lazima yasonge mbele. Mtataniwa sana, Mtachorwa sana, Mtaambiwa kila kitu cha karaha na maudhi, ila jueni maumivu haya sio ya milele"
"Nawaomba na kuwasihi mtulie na kujipanga,tumeshafeli lakini sio mwisho wa dunia"
"Na mtambue jitihada hazizidi kudra, tugange yajayo sasa"
ADVERTISE HERE