Okwi, Kotei watajwa sare ya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Aug 2019
Okwi, Kotei watajwa sare ya Simba

Simba imeondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya UD Songo hapo jana

Matokeo hayo sio kwamba yamewaumiza mashabiki tu, bali yamewafanya wakikumbuke kikosi chao cha msimu uliopita

Mchezaji aliyekumbukwa sana ni Mganda Emmanuel Okwi aliyetimkia Misri

Uwepo wa Okwi kwenye kikosi cha Simba msimu uliopita ulimnufaisha sana Meddie Kagere kwani kazi ambayo anaifanya sasa ilikuwa ikifanywa na mganda huyo

Okwi ni msumbufu na anajua kulazimisha makosa kwa mabeki. Aina yake ya uchezaji ilimpa Kagere nafasi ya kuwa huru na kufunga kila mara

Aidha kukosekana kwa nahodha John Bocco ambaye ni majeruhi pia ilikuwa changamoto

Kiungo James Kotei ni mchezaji mwingine ambao wengi hawaamini uamuzi wa uongozi wa Simba kumuacha

Hata kocha Patrick Aussems aliwahi kulizungumza hili, kuwa hakupenda Okwi na Kotei waachwe

Kotei alikuwa akifanya kazi isiyoonekana Simba, alikuwa ni mlinzi wa safu ya ulinzi ya Simba

Kazi yake kubwa ilikuwa kufuta makosa ya safu ya ulinzi na wakati mwingine alidhibiti yasitokee

Kwa sasa Simba ina viungo wengi wazuri wa kushambulia lakini katika ulinzi hawako bora sana

Shiboub alianza vizuri sana, lakini baadae alishindwa kuonyesha makali yake pengine presha ya mchezo ilimfanya ashindwe kutamba. Aussems alilazimika kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Miraji Athumani

Wengi wana matumaini makubwa kwa kiungo Mkenya Francis Kahata lakini nae siku ya jana mchezo ulimkataa na Aussems kulazimika kumtoa baada ya dakika 40

Simba imetolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambayo uongozi uliwekeza sana kufanya vizuri

Nguvu hii sasa ihamishiwe kwenye ligi na kombe la FA

Kwa kikosi kilichopo, Simba ina kila sababu ya kushinda makombe yote mawili

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’