Matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya UD Songo jana yaliivurugia Simba mipango ya kusonga mbele michuano ya ligi ya mabingwa
Ni matokeo yaliyowaumiza sana mashabiki, lakini kwa hakika wachezaji na benchi la ufundi waliumia zaidi
Simba ilikuwa bora sana jana hasa kwenye kipindi cha pili, lakini wakati mwingine mpira una matokeo ya kikatili sana
Sidhani kama yupo anayepaswa kulaumiwa miongoni mwa wachezaji kwani walipambana sana, kilichokosekana ni matokeo tu
Nyakati kama hizi hutokea wakati mwingine
Jana baada ya mchezo, viongozi wa benchi la ufundi walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwarejesha wachezaji kwenye hali ya kawaida
Hakika matokeo haya yamewaumiza sana
Ni nadra sana kumuona mashambuliaji jasiri kama Meddie Kagere akitokwa na machozi, lakini kilichotokea jana kimemliza kila mtu
Uongozi wa Simba unapaswa kuwajenga kisaikolojia wachezaji ili warejee katika hali ya ushindani kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania siku ya Alhamisi
Matokeo haya yamewaumiza lakini inapaswa wasaidiwe ili wayasahau haraka, yasije kuathiri ushiriki wa timu kwenye ligi ambayo imeanza juzi
Njia pekee ya kupunguza machungu haya ni kuhakikisha Simba inaibuka na ushindi mnono kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania August 29