Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kuondoshwa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa ni matokeo yaliyowaumiza sana
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya UD Songo ambao umemalizika kwa sare ya bao 1-1, Aussems amesema wachezaji wake hawakucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza
Hata hivyo amesema kipindi cha pili walikuwa imara na walitengeneza nafasi nyingi, lakini bahati haikuwa upande wao
Amesema wanapaswa kusahau matokeo hayo na kujikita kwenye michuano mingi ambayo watashiriki hapa nchini
"Ni matokeo yaliyotuumiza, lakini nimeridhishwa na mchezo tulioonyesha kipindi cha pili, kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri"
"Imekuwa bahati mbaya kwetu, msimu uliopita ulikuwa wa furaha kwetu lakini msimu huu umekuwa na huzuni kwenye michuano hii"
"Tunajipanga kufanya vizuri kwenye michuano mingine ambayo tutashiriki hapa nchini"