Aussems apania kulinda rekodi ya Simba nyumbani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Aug 2019
Aussems apania kulinda rekodi ya Simba nyumbani

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamejiandaa kupata ushindi mchezo dhidi ya UD Songo, ukiwa ni mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambao utapigwa keshokutwa Jumapili, August 25 2019 katika uwanja wa Taifa

Aidha Aussems amesema wanapocheza nyumbani, sapoti ya mashabiki imekuwa chachu kwa wao kufanya vizuri

Amesema wana wajibu wa kulinda rekodi waliyoweka msimu uliopita kwa kutopoteza mchezo uwanja wa Taifa

Lakini pia kuvuka hatua waliyofika msimu uliopita

"Utakuwa mchezo mgumu, hata hivyo malengo yetu ni kupata ushindi. Tumejiwekea malengo ya kuvuka hatua tuliyofikia msimu uliopita," amesema

"Mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani, washuhudie kile tunachoenda kufanya"

Msimu uliopita Simba iliondoshwa hatua ya robo fainali ikifungwa na TP Mazembe mabao 4-1

Ilishinda michezo mitano dhidi ya Mbabane Swallows, Nkana Fc, JS Soura, Al Ahly na AS Vita huku ikilazimishwa suluhu ya bila kufungana na TP Mazembe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’