Kiungo wa AS Kigali Haruna Niyonzima amesema anaamini Simba itaifunga UD Songo Jumapili na kusonga mbele hatua inayofuata michuano ya ligi ya mabingwa harani Afrika
Niyonzima aliyetembelea mazoezi ya Simba leo, amesema msimu uliopita walijiwekea malengo kuwa hakuna kupoteza mchezo nyumbani
"Sisi msimu uliopita tulijiwekea malengo kuwa hakuna kufungwa mchezo wowote nyumbani na tulifanikiwa," amesema
"Kama Simba bado ina morali ileile nafikiri hakuna timu itaweza kuwafunga hapa Tanzania"
"Muhimu ni mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenda kuipa sapoti timu yao kama walivyofanya mwaka jana"
Niyonzima yuko nchini na timu ya AS Kigali ambayo Ijumaa itacheza na KMC kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho
ADVERTISE HERE