Shirikisho la soka Barani Afrika limebainisha kuwa klabu ya Simba ndio iliyoweka rekodi msimu uliopita kwa kujaza mashabiki kwenye michezo yake ya nyumbani
Takwimu hizo iwe chachu ya Wanamsimbazi kujitokeza kwa wingi Jumapili kwenye mchezo dhidi ya UD Songo
Ukiacha ubora wa timu, mashabiki wa Simba ni sababu nyingine ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kupata mafanikio makubwa msimu uliopita
Kwa nyomi la Wanamsimbazi, hakuna namna kuna timu inaweza kutoka salama uwanja wa Taiifa
Viingilio vya mchezo wa Jumapili vimewekwa hadharani jana ambapo bei ya chini kabisa, Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B na C Tsh 15,000/-, VIP A 30,000/- PLatinum Tsh 100,000/- na Platinum Plus ni Tsh 150,000/-
Tiketi zinapatikana kupitia Selcom (kwa wenye kadi) wakati tiketi za karatasi zitaanza kuuzwa Ijumaa, August 23