Wachezaji Simba wajazwa mamilioni baada ya kuichapa Azam Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2019
Wachezaji Simba wajazwa mamilioni baada ya kuichapa Azam Fc

Nyota wa Simba mbali ya kuonekana kuwa na furaha kwa kufungua vizuri msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam FC, mabao 4-2, lakini kuanza leo Jumatatu muda wote akaunti zao zitajazwa noti.

Hii ni baada ya mabosi wa klabu hiyo kuahidi mapema kwamba wangewamwagia mamilioni kama wangeinyoosha Azam ikiwa sehemu ya utartibu waliojiwekea tangu msimu uliopita na kwa ushindi wa juzi Jumamosi usiku nyota hao watavuta Sh 50 milioni

Mgawanyo wa fedha hizo ni kwamba waliocheza kila mmoja atachukua si chini ya Sh 2 milioni, huku wale walioishia benchi kama kipa Ally Salimu watavuta si chini ya Sh 1 milioni na wale ambao waliishia kukaa jukwaani kama Ibrahim Ajibu watabeba si chini ya Sh 500,000.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema huo ni utaratibu ambao umewekwa katika timu yao ili wachezaji watamani kufanya vizuri katika kila mechi ili kuondoka na ushindi lakini inaongeza motisha kila mchezaji kutamani kushindana na kucheza katika kikosi cha kwanza.

"Ni utaratibu wetu ambao tunao tangu msimu uliopita katika mashindano yote ambayo tunashiriki kama tutashinda ujue kila mchezaji atapata motisha ya posho ila huwa zinatofautina kulingana na michezo husika kwani mechi nyingine ni kubwa na zinahitaji matokeo ya ushindi kuliko jambo lolote," alisema.

"Kuhusu ushindi wa hilo tayari limeshapita na akili zetu zipo katika mechi ya marudiano ambayo tutacheza Jumapili dhidi ya US Songo ambayo kiu yetu ni kuona tunashinda na kusonga katika hatua inayofuata.

"Kama vile ambavyo wachezaji na uongozi wanajitolea katika kuhakikisha wanawapa mashabiki furaha kwa kushinda mechi basi na wao wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mechi na UD Songo kama ambavyo tulifanya msimu uliopita ili kuendeleza wimbo la ushindi," alisema Magori.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
39m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’