Kipa wa Simba, Said Mohammed ‘Nduda’ aliyesajiliwa akitokea Mtibwa Sugar na kushindwa kuidakia timu hiyo hata mechi moja ya Ligi Kuu Bara, amerudi baada ya kupona jeraha lake la goti.
Nduda aliumia katika mazoezi ya kujianda na mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya watani zao Yanga wakiwa visiwani Zanzibar, maumivu yaliyomsababishia kwenda India kufanyia upasuaji. Kwa sasa amerudi mazoezini.
Kipa huyo aliyewahi kuzidakia Majimaji na Yanga, alianza mazoezi mepesi ya Gym tangu Jumatatu akisimamiwa na Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe.
“Nashukuru Mungu naendelea vizuri na nimeanza mazoezi maalumu kabla ya kufanya vipimo tena ili kuanza mazoezi ya mpira uwanjani,†alisema.
“Kwa jinsi ambavyo naendelea na imani kubwa kuwa si muda mrefu nitarudi uwanjani kwa ajili ya kuitumikia timu yangu ambayo sijaichezea hata mechi moja ya ligi tangu walivyonisajili.â€

ADVERTISE HERE