Majeraha ya Bocco yamtesa Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2019
Majeraha ya Bocco yamtesa Aussems

Wakati Simba ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo ambao utapigwa Jumapili ijayo, kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amesema itakuwa changamoto kama timu yake itamkosa nahodha John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc juzi

Aussems amesema wingi wa majeruhi kwenye kikosi chake unaweza kuwasumbua kuelekea mchezo huo

Bocco ameungana na wajeruhi wengine Aishi Manula, Ibrahim Ajib na Wilker Da Silva

Hata hivyo Manula, Ajib na Da Silva tayari wameanza mazoezi mepesi lakini Aussems amesema wana nafasi ndogo ya kucheza Jumapili

"Kuongezeka kwa majeruhi kunanipa kazi nyingine, kwa sababu walikuwa watatu, Ajib (Ibrahim), Wilker Da Silva, Aishi Manula na sasa ameongezeka Bocco"

"Madaktari wanaiangalia hali yake, natumaini hatakuwa ameumia sana"

cut

Pamoja na Bocco kuumia, Simba ilionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo dhidi ya Azam na kufanikiwa kushinda 4-2 na kutwaa Ngao ya Jamii kwa msimu wa tatu mfululizo

Aussems amesema amefurahi kutimiza lengo la kwanza msimu huu ambalo lilikuwa kutwaa Ngao ya Jamii

"Nimetimiza malengo yangu ya kuchukua Ngao ya Jamii mara ya pili, lakini mechi pia ilikuwa ni maandalizi ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa na UD Songo"

"Nimefurahishwa na kiwango cha wachezaji wangu japo kuna mapungufu nimeyaona, nitayafanyia kazi kwa siki hizi zilizobaki ili kukaa sawa kwa sababu mechi ijayo ni muhimu kushinda"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’