Manula amsifu Kakolanya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Aug 2019
Manula amsifu Kakolanya

Mlinda lango wa Simba Aishi Manula amesema hana shaka na uwezo wa Beno Kakolanya na amevutiwa na kiwango alichoonyesha jana kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc

Manula ambaye kwa sasa bado yuko nje akiendelea na matibabu ya majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu ya taifa, amesema Simba ilimsajili Kakolanya kwa kuwa walifahamu anao uwezo wa kucheza timu hiyo

"Siku zote huwa nikimuangalia Kakolanya namuona ni kipa mzuri sana, Simba ilimsajili kwa kuwa walimuona ana uwezo," amesema

Manula amesema kufanya vizuri kwa Kakolanya ni jambo zuri kwa klabu ya Simba kwani aliletwa ili kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake

"Nikiwa langoni mimi, Kakolanya au Salim ni sawa tu kwani sote lengo letu ni moja, kuhakikisha timu inapata ushindi na kufikia malengo yake"

Uimara unaoonyeshwa na Kakolanya wakati huu ambao Manula ni majeruhi, huenda ukampa changamoto baadae kwani Manula atalazimika kufanya kazi ya ziada kurejesha 'ufalme' wake

Hata hivyo ushindani huo utainufaisha zaidi Simba kwani wachezaji hao watafanya kazi mara dufu ili waendelee kuaminiwa

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’