Wawa, Nyoni watahadharishwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Aug 2019
Wawa, Nyoni watahadharishwa

Licha ya ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc jana, safu ya ulinzi ya Simba iliyokuwa ikiongozwa na wakongwe Paschal Wawa na Erasto Nyoni ilifanya makosa kadhaa ambayo yangeweza kuwagharimu mabingwa hao wa Tanzania

Mara kadhaa Azam Fc ilifanikiwa kupitisha mipira nyuma ya walinzi hao na kuwapa nafasi washambuliaji wa Azam kuonana ana kwa ana na mlinda lango Beno Kakolanya

Mara mbili mshambuliaji wa Azam Fc Shabani Iddi Chilunda alitumia udhaifu wa kutojipanga vyema wa walinzi hao kuwatoroka

Kocha Patrick Aussema aliiona changamoto hiyo na alimzuia kiungo Jonas Mkude kupanda sana ili kusaidia majukumu ya ulinzi

Makosa yale hayapaswi kufanywa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Msimu huu Simba imefanyia sana kazi safu yake ya ulinzi ili kuhakikisha hairudii makosa ya kufungwa mabao mengi ugenini

Licha ya ujio wa walinzi wapya Wabrazil Tairone Da Silva, Gerson Fraga na Mtanzania Kennedy Wilson, bado wachezaji hao wameshindwa kumshawishi Aussems kuwatumia kwenye kikosi cha kwanza

Aussems ameendelea kuwategemea zaidi Wawa na Nyoni na mara chache akiwapa nafasi Fraga na Tairone

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’