Tulipaswa kushinda sita au saba - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Aug 2019
Tulipaswa kushinda sita au saba - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc

Hata hivyo amesema wangeweza kupata ushindi mnono zaidi kwenye mchezo huo kama washambuliaji wake wangekuwa makini

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo jana, Aussems alisema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake hata hivyo watafanya maboresho zaidi kabla ya kuivaa UD Songo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wiki ijayo

"Tulicheza vizuri, tulitengeneza nafasi nyingi, tungeweza kufunga mabao sita au saba kama washambuliaji wangu wangekuwa makini," amesema

"Hata hivyo bado tuna changamoto ya ulinzi wa mipira mirefu, tutaifanyia kazi kabla ya mchezo dhidi ya UD Songo"

Kuhusu majeraha ya nahodha John Bocco, Aussems amesema anasubiri ripoti wa daktari wa timu lakini litakuwa pigo kwa timu yake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa

"Natumaini hakuumia sana, tayari tuna wachezaji watatu majeruhi itakuwa tatizo kwetu kama nae atakaa nje kwa muda mrefu"

Baada ya ushindi huo, Simba inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD SOngo ambao utapigwa Jumapili iyao, August 25

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’