Inaelezwa klabu ya Simba tayari imeshampata mrithi wa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Crescentius Magori ambaye mkataba wake umemalizika
Ingawa bado uongozi wa Simba haujamtangaza rasmi, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini ndiye anayetajwa kuchukua nafasi yake
Jina la Mazingisa ni geni kwa hapa Tanzania lakini huko Afrika Kusini anafahamika sana
Amefanya kazi za uongozi katika vilabu kadhaa vinavyoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Miongoni mwa timu alizozitumikia ni pamoja na Platinum Stars na Orlando Pirates
uongozi wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo', umedhamiria kuisuka upya safu yake kwa kuweka watu wenye upeo mkubwa na kuiendesha timu hiyo kisasa
ADVERTISE HERE