Aussems apania taji la kwanza Ngao ya Jamii leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Aug 2019
Aussems apania taji la kwanza Ngao ya Jamii leo

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumamosi saa moja jioni watashuka uwanja wa Taifa kuikabili Azam Fc katika mchezo wa Ngao ya Jamii

Simba, mabingwa wa Ngao ya Jamii kwa misimu miwili mfululizo, watakuwa wakisaka rekodi ya kutwaa Ngao hiyo kwa msimu wa tatu

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali lakini amekiandaa kikosi chake vyema kuweza kutwaa taji la kwanza msimu huu

"Mchezo hautakuwa mwepesi, tunawaheshimu wapinzani wetu, tumewafuatilia wana timu nzuri. Mpango wetu ni kushinda ili tutwae taji la kwanza msimu huu," amesema

Kwenye mchezo huo, Simba itawakosa nyota wake watatu; Aishi Manula, Ibrahim Ajib na Wilker Da Silva ambao wameanza mazoezi juzi baada ya kupona majeraha

Wapinzani wao Azam Fc nao watawakosa wachezaji watatu Bruce Kangwa, Mudathir Yahya na Agrrey Moris wote wakiwa majeruhi

Huu utakuwa mchezo wa pili wa kimashindano kwa Simba msimu huu baada ya ule wa ligi ya mabingwa ambao ulipigwa Msumbiji

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’