Manara awaita mashabiki kuimaliza Azam Fc Ngao ya Jamii

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Aug 2019
Manara awaita mashabiki kuimaliza Azam Fc Ngao ya Jamii

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa

Kiingilio cha chini kabisa cha mchezo huo ambao utapigwa saa moja jioni ni Tsh 5,000/-

Manara amesema msimu huu Simba imejiwekea malengo ya kutwaa makombe ya michuano yote itakayoshiriki hapa nchini

"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi Jumamosi washuhudie kandanda safi kutoka kwa mabingwa wa nchi," amesema

"Tumeshachukua Ngao ya Jamii kwa misimu miwili mfululizo, tunataka kuchukua kwa mara ya tatu"

"Sisi lengo letu hasa ni kuchukua Ngao za Jamii kwa miaka 10 mfululizo kama ilivyo kwa ubingwa wa ligi kuu"

"Msimu huu ni wa makombe kwa Simba, tumejipanga kushinda mataji yote hapa nchini"

Alia na jezi feki

Katika hatua nyingine, Manara amezitaka mamlaka husika kudhibiti uingizwaji wa jezi feki ambazo mauzo yake yanadhoofisha mapato ya klabu

Manara amesema baada ya Simba kuzindua jezi mpya, kumejitokeza maharamia wanaoingia jezi feki

"Tumezitaka mamlaka husika zisimamie changamoto hii. Tumewaambia, kwa mzigo wowote wa jezi za Simba unaoingia Bandarini au sehemu nyingine, ni vyema wakawasiliana nasi kujiridhisha kama ni wetu au la"

"Kwani wanaoingiza jezi feki mizigo yao inapita hapo Bandarini au sehemu nyingine ambazo tunaamini Serikali inaweza kudhibiti"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
18h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’