Manula aitabiria Simba kufika mbali ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Aug 2019
Manula aitabiria Simba kufika mbali ligi ya mabingwa

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amesema uzoefu waliopata msimu uliopita kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, utawasaidia kufanya vizuri zaidi msimu huu

Manula aliyedaka mechi zote za Simba ligi ya mabingwa msimu uliopita, amesema wataendeleza pale walipoishia

Aidha mlinda lango huyo wa timu ya Taifa, amesema wanajivunia kuwa na mashabiki bora ambao wamekuwa wakiwahamasisha kufanya vizuri uwanja wa nyumbani

Amesema mchezo wa marudiano dhidi ya UD Songo, watafanya kile walichofanya kwenye michezo yote ya nyumbani msimu uliopita

"Naamini tutafanya vizuri tena msimu huu kutokana na uzoefu tulioupata katika mashindano haya msimu uliopita," amesema

"Nguvu ya mashabiki ni kubwa na hakika inatupa ari ya kushinda mchezo ujao dhidi ya UD Songo ambao utachezwa katika Uwanja wa taifa kwani naamini mashabiki watakuja kwa wingi kutuunga mkono"

Manula ameanza msimu vibaya baada ya kupata majeraha wakati akjiitumikia timu ya Taifa

Anatarajiwa kurejea kikosini hivi karibuni baada ya kuanza mazoezi mepesi

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
12h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
12h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
15h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’