Wabrazil wanahitaji muda - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Aug 2019
Wabrazil wanahitaji muda - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesisitiza kuwa wachezaji wake raia wa Brazil, wanahitaji muda zaidi ili kuweza kuwa na mchango kwenye kikosi chake

Wakati mshambuliaji Wilker Da Silva akiwa majeruhi, walinzi Gerson Fraga na Tairone Sontos hawakupata nafasi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo uliopigwa Jumamosi iliyopita nchini Msumbiji

Aussems amesema hana wasiwasi na uwezo wa wachezaji hao lakini wanakabiliwa na changamoto ya kuzoea mazingira na utamaduni wa soka la Afrika

"Ni wachezaji wazuri lakini nadhani wanahitaji kuufahamu utamaduni wetu hapa na mazingira ya soka la Afrika kwa ujumla," amesema

"Kwa sasa tusitarajie mambo makuwa sana kutoka kwao"

Aidha Aussems amesema kwa ujumla kikosi chake kina wachezaji wageni asilimia 50 hivyo baadhi wanahitaji muda zaidi ili kuweza kwenda sambamba na wenzao waliowakuta

Jumamosi ya August 17 Simba itacheza na Azam Fc mchezo wa Ngao ya Jamii kisha kuikaribisha UD Songo kwenye dimba la Taifa August 25 kwenye mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’