Aussems hana wasiwasi kabisa na UD Songo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Aug 2019
Aussems hana wasiwasi kabisa na UD Songo

Kocha Mkuu wa Simba,  Patrick Aussems , amesema anaamini kikosi chake kitatumia vizuri ardhi ya nyumbani kuiondosha mashindanoni UD Songo na kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba juzi ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya UD Songo ya Msumbuji, katika mchezo  wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Jiji la Kibiashara la Beira, Msumbiji.

Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo, utachezwa  Agosti 25 mwaka huu,   Uwanja wa taifa,  Jijini Dar es Salaam.

Ili kusonga mbele, Simba inahitaji ushindi,huku wapinzani wao wakihitaji matokeo ya sare ya mabao kwa kuzingatia kigezo cha bao la ugenini.

Aussems alimesema walikusudia kupata ushindi ugenini, lakini wakakwama na sasa wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani.

Alisema,  amewasoma vizuri wapinzani wao na kubaini kasoro kadhaa ambazo ana amini watazitumia kupata ushindi katika mchezo wa marudiano.

"Sina muda wa kupoteza tena ndio maana tumerudi na kuanza mazoezi haraka,  hii michuano ni migumu," Aussems aliliambia Mtanzania

"Ili kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele tulipaswa kushinda ugenini na nyumbani. Jambo la kujivunia ni kwamba nyumbani tutacheza tukiwa na mashabiki wetu ambao wana maana kubwa katika kufanikisha ushindi wetu"

"Pia unaweza kuona mazingira ya uwanja tuliochezea mechi ugenini ni tofauti na Taifa ambao unaruhusu kuucheza mchezo wetu"

Aussems  amesema tofauti na msimu uliopita ambapo malengo yalikuwa kufika hatua ya makundi lakini wanafanikiwa kufika robo fainali, safari hii  wamejiandaa kwa mapambano ya kuwania ubingwa.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’